TENZI ZA ROHONI NO. 158
____________________________________________
Aniongozapo pote,
Nimwandame Siku zote.
Kwa ajili yangu Mimi
Aliuawa kalvari.
Nitaongozwa na Bwana
Usiku kucha na Mchana,
Yesu, Rafiki wa heri;
Ninakumbuka kalvari.
Lanitosha neno lake,
Nishikwe na mkono wake.
Mapenzi yake ni heri,
Yalitimizwa kalvari.
Nitaendelea mbele
Pamoja naye milele.
Pendo lake ni hiari,
Bwana Yesu wa kalvari.
No comments:
Post a Comment