Search This Angaza Gospel

Tuesday, 8 December 2020

BWANA MUNGU Nashangaa kabisa.

Roho yangu na ikuimbie,Jinsi wewe ulivyo Mkuu, Roho yangu naikuimbie Jinsi wewe ulivyo Mkuu. 
__________________________________________
NYIMBO ZA WOKOVU no.300

1.Bwana Mungu, nashangaa kabisa, 
Nikifikiri Jinsi ulivyo, 
Nyota, ngurumo, vitu vyote pia, 
Viumbwavyo kwa uwezo wako. 

Roho yangu na ikuimbie, Jinsi wewe 
Ulivyo Mkuu. Roho yangu na ikuimbie, 
Jinsi wewe ulivyo mkuu. 

2.Nikitembea pote duniani, 
Ndege huimba nawasikia. 
Milima hupendeza Macho sana, 
Upepo nao nafurahia. 

3.Nikikumbuka vile wewe Mungu, 
Ulivyom-peleka mwanao, 
Afe azichukue dhambi zetu, 
Kuyatambua ni vigumu mno. 

4.Yesu mwakozi utakaporudi, 
Kunichukua kwenda mbinguni, 
Nitaimba sifa zako milele, 
Wote wajue jinsi ulovyo. 

No comments:

Post a Comment